December 28, 2016

MAMBO SITA YA KUZINGATIA WAKATI WA UCHAGUZI ENEO LA BUSTANI


 MAMBO SITA YA KUZINGATIA WAKATI WA UCHAGUZI ENEO LA BUSTANI

Kwa mafanikio ya kilimo cha bustani ni muhimu sana kuzingatia uchaguzi wa eneo, hii itapelekea zao Fulani kutoa mazao mazuri kutokana na uchaguzi mzuri wa eneo, kwa kuzingatia sifa zifuatazo za eneo hilo.
Chagua eneo lenye sifa zifuatazo.

1.HALI YA HEWA.
Hali ya hewa hapa vipengele vifuatavyo vinahusishwa joto (Temperature), mvua (rainfall) kiasi cha unyevu katika anga (humidity), kasi ya upepo (wind), zote hizi ni vitu vya kuzingatia sana katika uchaguzi wa eneo, mazao mengi yana mahitaji tofauti ya hali ya hewa hivyo kukufanya ewe mkulima kuwa mwangalifu katika hill.
2.AINA YA ZAO
Aina ya zao pia ni kitu kingine cha muhimu sana, mazao na eneo hupelekea mafaniio ya kilimo sio mazao yote yanaleta fauda kubwa hivyo chagua zao ambalo litaendana na faida kwa kushirikisha na uchaguzi wa eneo pamoja na soko lako.

3.CHANZO CHA MAJI.
Maji ni uhai wa bustani na maji hayo yawe na sifa zifuatazo yawe yanapatikana kwa kipindi chote cha msimu wa uzalishaji, maji yawe yenye ubora na sio yaliyo changanyika na kemikali, ambazo huenda yakaleta madhara kwa matumizi ya binadamu.

4.UPATIKANAJI WA VIBARUA.
Wafanyakazi kwaajili ya kufanya shughuli mbalimbali za shamba ikiwemo palizi, upuliziaji wa dawa shamba na hata uvunaji.

5.URAHISI KUFIKA SOKONI.
Ufikaji wa mazao sokoni ni jambo pia la kuzingatia, kuanzia usafirishaji.

6.AINA YA UDONGO.
Kila zao lina aina yake ya udongo kwaajili uzalishaji utakaoleta mazao mazuri, hivyo zingatia sana aina ya udongo, kuna aina kuu tatu za udongo mfinyanzi, kichanga, na tifutifu,
Udongo wa mfinyanzi hufaa sana mazao kama kitunguu, mpunga kwani udongo huu hutuamisha sana maji, udongo wa kichanga hufaa kwa mazao kama karroti, udongo wa tifutifu huu ni udongo ambao mazao mengi hustawi sana kwani ndio udongo unaoshauriwa sana kitaalamu kwa mavuno bora.

August 23, 2016

CUF KUTUA KWA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA





WAFUASI wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, wametangaza kwenda kwa Msajili wa Vyama vya Siasa kuwasilisha malalamiko yao ya kupinga utaratibu uliofanywa na wajumbe wa Mkutano Mkuu cha chama hicho.
Wakati wanachama hao wanaomuunga mkono Prof. Lipumba wakidai hayo, CUF imetoa msimamo wake na kusema kuwa imeshamalizana na kiongozi huyo na kilichobaki sasa ni kujiandaa kujaza nafasi za uongozi zilizo wazi.
Taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mawasiliano ya Umma, Salim Bimani, ilieleza kuwa wajumbe wengi wa Mkutano Mkuu Maalumu uliofanyika juzi walipiga kura ya kuridhia kujiuzulu kwa Prof. Lipumba na kwamba mchakato wa kujaza nafasi hizo utafanyika.
“Ni muhimu kukumbuka kwamba ajenda ya kwanza ya msingi katika Mkutano Mkuu imekamilika kwa wajumbe wengi kukubali kujiuzulu kwa mheshimiwa Prof. Lipumba.
“Mchakato wa kukamilisha zoezi la kujaza nafasi wazi za uongozi wa chama taifa upo palepale na baada ya kukamilisha taratibu za ndani ya chama, tutatoa taarifa kwa Watanzania wote.
“Chama kinapenda kuwataarifu na kuwahakikishia wanachama, wapenzi wa chama chetu na marafiki zetu wote kuwa hii ni taasisi kubwa ya kisiasa nchini iliyo na viongozi makini na mahiri,” alisema Bimani.
Mkurugenzi huyo wa uenezi, alisema kuwa mchakato wa kumwondoa rasmi Prof. Lipumba katika nafasi yake ulifanyika kwa mujibu wa katiba ya chama hicho.
Alisema kura zilipigwa baada ya kutimia kwa akidi ya wajumbe halali waliopaswa kuhudhuria mkutano huo, na kwamba kwa mujibu wa Katiba ya CUF ya mwaka 1992 ibara ya 79(3) toleo la mwaka 2014, walipaswa kumchagua mwenyekiti atakayesimamia zoezi hilo.
“Baada ya kuona akidi imetimia, wajumbe walimchagua Julius Mtatiro kusimamia suala la upigaji wa kura, ambapo waliotaka Prof. Lipumba aondoke walikuwa 476 na waliopinga walikuwa wajumbe 14, huku wengine wakikataa kupiga kura,” alisema Bimani.
Aliongeza kuwa kutokana na hali hiyo, Prof. Lipumba si mwenyekiti tena wa chama hicho, na kwamba wanachama wanapaswa kuwa watulivu katika kipindi hiki, na kuzipuuza taarifa zote zenye lengo la kupotosha usahihi wa suala hilo.

WATETEZI WA LIPUMBA
Kutokana na uamuzi huo, wafuasi wanaomuunga mkono Prof. Lipumba, wamepinga uamuzi huo na kutangaza kwenda kwa Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, kueleza kilichotokea ikiwamo kuvunjwa kwa utaratibu.
Akizungumza na MTANZANIA nje ya Ofisi Kuu ya CUF, Buguruni Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa CUF Wilaya ya Serengeti, Joseph Magoiga, alisema kura zilizopigwa si halali kwa sababu hazikuwa za siri kwa mujibu wa Katiba ya CUF.
Alisema kitendo hicho ndicho kilichosababisha vurugu, huku wajumbe wengine wakisusia utaratibu huo na kutoka nje ya ukumbi wa mkutano.
“Mtatiro aliwaambia wajumbe wanaomtaka Profesa Lipumba kunyoosha vidole juu ili aweze kuwahesabu, lakini sisi tulisimama wote na kusema hatutaki kwa sababu katiba ya chama inataka kupiga kura za siri na si ya kunyoosha vidole juu,” alisema Magoiga na kuongeza:
“Pamoja na wajumbe kugoma kupiga kura, lakini  Maalim Seif (Sharif Hamad, Katibu Mkuu CUF) alimwambia Mtatiro aendelee kuhesabu wajumbe walionyoosha mkono na akatangaza matokeo katika hali ya vurugu. Kutokana na hali hiyo jana (juzi) tuliorodhesha majina zaidi ya 300 ya wajumbe wa Tanzania bara, tutakwenda kwa Msajili wa Vyama vya Siasa ili tuweze kumweleza kilichotokea ndani ya mkutano huo.
“Suala hili tutalifanya pamoja na kumwandikia barua ya kupinga uamuzi uliotolewa na Maalim Seif pamoja na watu wake,” alisema Magoiga.

MTATIRO AELEZA
Kwa upande wake, aliyekuwa Mwenyekiti wa muda wa Mkutano Mkuu huo, Mtatiro, jana alitoa taarifa huku akieleza mambo 15 yaliyotokea.
Alisema akidi ilitimia kwa pande zote – bara na Zanzibar, na alichaguliwa kwa kura zaidi ya 500 kuwa mwenyekiti wa muda. Aliyemfuatia alikuwa ni Ridhiwani wa Morogoro aliyepata kura 170.
“Baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CUF wapatao 10 kutoka Tanzania Bara walitoa hoja zao kwa kutaka kikao kimwite Prof. Lipumba ili aje ajieleze kuhusu kujiuzulu kwake jambo ambalo lilipingwa na wajumbe wengine,” alisema.
Alisema alipowataka wajumbe wanaotaka Lipumba aletwe kueleza kifungu cha katiba au kanuni kinachotaka hivyo walishindwa kueleza.
Kwa upande wa wajumbe waliokataa Prof. Lipumba kufika mkutanoni, alisema walinukuu ibara ya 117(2) ambayo inataka taarifa ya kujiuzulu kwake ndiyo ipelekwe kwenye mkutano mkuu na si yeye mwenyewe.
Alisema aliujulisha mkutano kuwa Prof. Lipumba si mjumbe wa kikao, kwa hiyo hawezi kuitwa na kwamba mkutano ujadili barua zake na ufanye uamuzi wa kumrudisha au kutomrudisha.
“Baadhi ya wajumbe wa mkutano mkuu kutoka Tanzania Bara walikataa mkutano usifanye maamuzi yoyote, huku wengine wakitaka maamuzi yafanyike.
“Kwa hiyo Tanzania Bara iligawanyika nusu kwa nusu kwenye jambo hilo. Hofu ya wajumbe wa Bara waliokataa maamuzi yasifanywe ilikuwa ni kuwa yakifanyika yataathiri mipango yao,” alisema Mtatiro.
Alisema wakati wakijadiliana suala hilo, Prof. Lipumba alijitokeza akiwa na kundi la mabaunsa wapatao 30 wakisindikizwa na ofisa wa polisi aliyekuwa na ‘radio call’.

July 21, 2016

Mbinu Kumi(10) Za Kuwafanya Wateja Waendelee Kufanya Biashara Na Wewe


Mbinu Kumi(10) Za Kuwafanya Wateja Waendelee Kufanya Biashara Na Wewe.
Kazi kubwa sana unayohitaji kufanya baada ya kumpata mteja ni kuhakikisha anaendelea kuwa wako, yaani anaendelea kufanya biashara na wewe.
Wafanyabiashara wengi wamekuwa wakitumia nguvu kubwa kuwafikisha wateja kwenye biashara zao, lakini wateja wanapofika na kupata huduma huondoka na wengi kutokurudi tena.
Ni rahisi sana kumuuzia mteja ambaye ulishamuuzia awali, kuliko kumuuzia mteja mpya. Hivyo kama ukiweza kuiendesha biashara yako vizuri, wateja ambao wananunua kwako watakuwa wateja wako wa kudumu.

Zifuatazo ni mbinu kumi unazotakiwa kuanza kuzitumia leo kwenye biashara yako ili kuhakikisha wateja wako wanaendelea kufanya biashara na wewe.
1. Tekeleza ulichoahidi.
Kama umemtangazia mteja kwamba akija kwenye biashara yako atapata kitu fulani, basi hakikisha anapata kitu hiko. Hakuna kitu ambacho watu hawapendi kama kudanganywa. Mteja anapoona kwamba amedanganywa hatorudi tena kwenye biashara yako na utakuwa umemkosa milele. Hakikisha unatimiza ulichomwahidi mteja wako.
2. Ahidi kikubwa na pitiliza(overpromise and overdeliver)
Najua hapa unaweza usielewe kwa sababu ulichozoea ni kuahidi kidogo na kupitiliza(underpromise and overdeliver). Hii ilikuwa unafanya kazi zamani, ila kwa sasa, haifanyi kazi tena. Kwa sababu kama wewe unaahidi kidogo, wenzako wanaahidi kikubwa na wanafanyia kazi. Hivyo kitu pekee cha kuhakikisha unawabakisha wateja ni kuwaahidi makubwa na kuyapitiliza hayo. Kama umejitoa kweli kwenye biashara yako, hili halitakushinda.
3. Imarisha mawasiliano yako na wateja wako.
Ni muhimu sana uwe na mawasiliano na wateja wako. Bila ya kujali ni biashara gani unafanya, kuna na mfumo w akupata namba za simu, au barua pepe za wateja wako. Mata kwa mara watumie ujumbe ukiwatakia heri na wakati mwingine kuwajulisha bidhaa au huduma mpya zilizopo kwenye biashara yako.
4. Fanyia kazi malalamiko ya wateja haraka.
Wateja wanapokuwa na malalamiko, yafanyie kazi haraka sana. Usisubiri mpaka yawe makubwa kiasi cha kuwafanya watafute mahali pengine wanakoweza kufanya biashara bila ya matatizo wanayopata kwako.
5. Toa huduma bora ambazo mteja hawezi kupata popote.
Huduma kwa wateja, mteja amepokelewaje, ameelezwaje kuhusiana na bidhaa au huduma anayohitaji, maswali yake yamejibiwaje, hivi ni vitu vinavyoonekana vidogo sana ila vina maana kubwa sana kwa wateja wa biashara yako. hakikisha wateja wako wanapata huduma ambazo zitawafanya wajisikie ufahari.
6. Wakumbuke wateja waliopotea.
Kama biashara yako imekuwepo kwa muda, kuna wateja waliokuwepo awali ila kwa sasa hawapo tena. Kuna wateja ulikuwa unafanya nao biashara zamani, ila kwa sasa huwaoni tena kwenye biashara yako. ni vyema kuwatafuta na kujua kwa sasa biashara wanafanya na nani na ni kitu gani limewafanya hawaji tena kwako.
7. Muuzie mteja baada ya kumuuzia.
Mara nyingi mteja atakuja kwako akitaka kitu fulani, lakini pia anaweza kuwa anataka vingine zaidi ya alichofuata hapo. Ni jukumu lako kujua mahitaji haya yote ya mteja wako na kuyafanyia kazi. Usiishie kumuuzia mteja kitu kimoja pekee, hakikisha kila anachohitaji ambacho kipo kwenye biashara yako, unampatia. Ataendelea kuja kwako kwa sababu anajua mahitaji yake yote anayapata kwako.
8. Pima thamani ya mteja ya muda mrefu.
Kuna wateja ambao wananunua mara moja na kuondoka na kuna wateja ambao wataendelea kununua kwako kwa muda mrefu. Wateja wanaonunua mara moja na kuondoka unaweza kupata faida kubwa, lakini ndio imeishia hapo. Wateja ambao wananunua muda mrefu unaweza kupata faida ndogo, ila utaendelea kuipata kwa muda mrefu. Jua wateja wale wa muda mrefu na endelea kuwapatia thamani nzuri.
9. Tumia mtandao wa intaneti na mitandao ya kijamii kuwa karibu na wateja wako.
Mtandao umerahisisha sana mfanyabiashara kuwa karibu na wateja. Hakikisha biashara yako ipo kwenye mtandao kwa kuwa na tovuti, kuwa na blogu na kuwa na kurasa kwenye mitandao ya kijamii. Utatumia mitandao hii kutoa taarifa muhimu kuhusiana na biashara yako.
10. Toa zawadi na motisha kwa wateja.
Kuwa na njia ambapo utatoa zawadi mbalimbali kwa wateja wanaorudi tena kwenye biashara yako. inaweza kuwa kuwapatia kuponi za punguzo kadiri wanavyonunua mara nyingi, au kutoa punguzo la bei kama mteja ananunua mara nyingi. Vyovyote vile hakikisha mteja anapata motisha pale anaponunua kwako kwa muda mrefu.

kwa ushauri wa kibiashara piga 0713735601 au email johnhmwende@yahoo.com 

June 13, 2016

'Waislamu hawafai kuingia Marekani' -Trump


'Waislamu hawafai kuingia Marekani' -Trump

Image copyrightAP
Image caption'Waislamu hawafai kuingia Marekani' -Trump
Mgombea wa kiti cha urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump, amesema mauaji ya watu 50 katika baa moja ya wapenzi wa jinsia moja huko Orlando inathibitisha msimamo wake kwamba waislamu wapigwe marufuku kukanyaga ardhi ya Marekani.
Trump amemkashifu mpinzani wake wa chama cha republican Bi Hillary Clinton, kwa kutodadisi sababu za mtu huyo kutenda mauaji hayo.
Image copyrightTWITTER
Image captionTrump amesema hatua kali zinapaswa kuchukuliwa dhidi ya waislamu
Upande wa Bi Clinton wakitoa risala za pole kwa waathiriwa wa mkasa huo papo hapo wamemtaja Trump kama mtoto anaejitweza ovyo kwa jinsi anavyougeuza mkasa huo wa kitaifa kujipongeza binafsi.
Image copyrightGETTY
Image captionWakati huo huo Shirika la kijasusi la FBI limesema mtu aliyewaua watu 50 kwa kuwafyatulia risasi katika klabu moja ya wapenzi ya jinsia alikiri kuunga mkono kundi la kigaidi la IS.
Wakati huo huo Shirika la kijasusi la FBI limesema mtu aliyewaua watu 50 kwa kuwafyatulia risasi katika klabu moja ya wapenzi ya jinsia alikiri kuunga mkono kundi la kigaidi la IS.
Image copyrightEPA
Image captionWatu 50 waliuawa katika shambulizi la risasi
Fbi wameongeza kusema kuwa wamekuwa wakimfanyia uchunguzi mtu huyo Omar Mateen tangu 2013 baada ya kutoa matamshi ya chuki akiwa kazini .
Image copyrightAFP
Image captionTrump amemkashifu mpinzani wake Hillary Clinton kwa utepetevu
Babake Mateen amesema anaamini kitendo alichokifanya wanawe kilitokana na msukumo wa hisia zake dhidi ya wanaondeleza mapenzi ya jinsia moja na wala si kwa sababu za kidini.
Naye mkewe wa zamani Sitora Yusufiy, amemwelezea Mateen kama mtu wa aliyekuwa tabia za kigomvi na kutaka kupiga watu lakini hakuwa na itikadi kali za kidini.

Bill Gates kusaidia watu kufuga kuku Afrika


Bill Gates kusaidia watu kufuga kuku Afrika

Mwanzilishi wa kampuni ya Microsoft Bill Gates, amezindua kampeni ya kusaidia watu maskini zaidi barani Afrika, kusini mwa jangwa la sahara, kwa kufuga kuku
Bilionea huyo Bill Gates anasema kuwa kufuga kuku kunaweza kuwa kifaa muhimu katika kukabiliana na ufukara hohe hahe.
Ameahidi kutoa kuku 100,000, na ukurasa katika mtandao wa mradi huo tayari umewavutia na kusambazwa kwa maelfu ya watu.
Umoja wa Mataifa unakisia kuwa asilimia 41 ya watu katika Bara la Afrika, Kusini mwa jangwa la Sahara wanaishi katika ufukara mkubwa.
Image captionBwana Gates alisema kuwa mkulima anayefuga kuku watano anaweza kupata zaidi ya Dola 1,000 kwa mwaka.
Bwana Gates alisema kuwa mkulima anayefuga kuku watano anaweza kupata zaidi ya Dola 1,000 kwa mwaka. Mtu hutajwa kuwa maskini iwapo anapata Dola 700 pekee kwa mwaka.
Alisema kuwa lengo la mradi huo ni kusaidia zaidi ya asilimia 30 ya watu wanaoshi mashambani Kusini mwa Jangwa la Sahara ili wapate huduma ya kufuga kuku wa hali ya juu mbao watachanjwa. Alisema hatua hiyo itaongeza watu wanaofuga kuku kwa asilimia tano.
Ananukuliwa akisema kuwa kuku huongezeka maradufu na kwa hivyo hakuna uekezaji ulio na mapato mazuri kwa asilimia ya juu kuliko ufugaji kuku.
Alisema hayo alipokuwa akianzisha mradi huo jijini New York. Anashirikiana na shirika na kutoa misaada kwa maskini la Heifer International.
Watu milioni 800 huishi katika hali ya umaskini hohehahe, kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa.

Aliyewaua watu Florida alikiri kuunga IS mkono


Aliyewaua watu Florida alikiri kuunga IS mkono


Image copyrightREUTERS
Image captionOmar Mateen

Shirika la ujasusi la Marekani- FBI, limesema mtu aliyewaua watu 50 kwa kuwafyatulia risasi katika klabu moja ya wapenzi ya jinsia moja huko Florida, alikiri kuunga mkono kundi la kigaidi la IS, lakini hawakumuona kama mtu hatari.
Mateen, anasemekana kupigia simu mamlaka ya kitaifa ya maswala ya dharura muda mfupi kabla ya kuanza kuwapiga watu risasi huku akisema kuwa anaunga mkono kundi la IS.
FBI wameongeza kusema kuwa wamekuwa wakimfanyia uchunguzi mtu huyo tangu 2013 baada ya kutoa matamshi ya chuki akiwa kazini.

Image copyrightEPA
Image captionEneo la mkasa

Wakati alipotoa matamshi hayo ya chuki, alikuwa na uhusiano na mhanga mmoja aliyejilipua nchini Syria.
Mateen aliendelea kufanya kazi kama mlinzi wa usalama huku akinunua silaha kisheria.
Babake Mateen amesema anaamini kitendo alichokifanya mwanawe kilitokana na msukumo wa hisia zake dhidi ya wanaondeleza mapenzi ya jinsia moja na wala si kwa sababu za kidini.

Magufuli awaapisha Nchemba na Tizeba


Magufuli awaapisha Nchemba na Tizeba
Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewaapisha mawaziri wapya wa mambo ya ndani na yule wa kilimo siku mbili tu baada ya kutangaza mabadiliko madogo katika baraza lake la mawaziri.
 

Jumamosi iliyopita rais Magufuli alitangaza uteuzi wa mbunge wa Buchosha Dkt. Charles John Tizeba kuwa waziri wa kilimo, mifugo na uvuvi.
Kufuatia uteuzi huo, aliyekuwa Waziri wa Kilimo, bwana Mwigulu Lameck Nchemba aliteuliwa kuwa Waziri wa mambo ya ndani ya nchi.
Image captionRais Magufuli ampongeza waziri Nchemba kwa wadhifa wake mpya
Bwana Nchemba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani bw Charles Muhangwa Kitwanga ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.
Mawaziri hao walikula kiapo cha uaminifu kwa rais na jamhuri ya tanzania saa tatu asubuhi katika ikulu ya rais jijini Dar es salaam.

Harmonize Ft Diamond Platnumz Kwangwaru