June 13, 2016

'Waislamu hawafai kuingia Marekani' -Trump


'Waislamu hawafai kuingia Marekani' -Trump

Image copyrightAP
Image caption'Waislamu hawafai kuingia Marekani' -Trump
Mgombea wa kiti cha urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump, amesema mauaji ya watu 50 katika baa moja ya wapenzi wa jinsia moja huko Orlando inathibitisha msimamo wake kwamba waislamu wapigwe marufuku kukanyaga ardhi ya Marekani.
Trump amemkashifu mpinzani wake wa chama cha republican Bi Hillary Clinton, kwa kutodadisi sababu za mtu huyo kutenda mauaji hayo.
Image copyrightTWITTER
Image captionTrump amesema hatua kali zinapaswa kuchukuliwa dhidi ya waislamu
Upande wa Bi Clinton wakitoa risala za pole kwa waathiriwa wa mkasa huo papo hapo wamemtaja Trump kama mtoto anaejitweza ovyo kwa jinsi anavyougeuza mkasa huo wa kitaifa kujipongeza binafsi.
Image copyrightGETTY
Image captionWakati huo huo Shirika la kijasusi la FBI limesema mtu aliyewaua watu 50 kwa kuwafyatulia risasi katika klabu moja ya wapenzi ya jinsia alikiri kuunga mkono kundi la kigaidi la IS.
Wakati huo huo Shirika la kijasusi la FBI limesema mtu aliyewaua watu 50 kwa kuwafyatulia risasi katika klabu moja ya wapenzi ya jinsia alikiri kuunga mkono kundi la kigaidi la IS.
Image copyrightEPA
Image captionWatu 50 waliuawa katika shambulizi la risasi
Fbi wameongeza kusema kuwa wamekuwa wakimfanyia uchunguzi mtu huyo Omar Mateen tangu 2013 baada ya kutoa matamshi ya chuki akiwa kazini .
Image copyrightAFP
Image captionTrump amemkashifu mpinzani wake Hillary Clinton kwa utepetevu
Babake Mateen amesema anaamini kitendo alichokifanya wanawe kilitokana na msukumo wa hisia zake dhidi ya wanaondeleza mapenzi ya jinsia moja na wala si kwa sababu za kidini.
Naye mkewe wa zamani Sitora Yusufiy, amemwelezea Mateen kama mtu wa aliyekuwa tabia za kigomvi na kutaka kupiga watu lakini hakuwa na itikadi kali za kidini.

Bill Gates kusaidia watu kufuga kuku Afrika


Bill Gates kusaidia watu kufuga kuku Afrika

Mwanzilishi wa kampuni ya Microsoft Bill Gates, amezindua kampeni ya kusaidia watu maskini zaidi barani Afrika, kusini mwa jangwa la sahara, kwa kufuga kuku
Bilionea huyo Bill Gates anasema kuwa kufuga kuku kunaweza kuwa kifaa muhimu katika kukabiliana na ufukara hohe hahe.
Ameahidi kutoa kuku 100,000, na ukurasa katika mtandao wa mradi huo tayari umewavutia na kusambazwa kwa maelfu ya watu.
Umoja wa Mataifa unakisia kuwa asilimia 41 ya watu katika Bara la Afrika, Kusini mwa jangwa la Sahara wanaishi katika ufukara mkubwa.
Image captionBwana Gates alisema kuwa mkulima anayefuga kuku watano anaweza kupata zaidi ya Dola 1,000 kwa mwaka.
Bwana Gates alisema kuwa mkulima anayefuga kuku watano anaweza kupata zaidi ya Dola 1,000 kwa mwaka. Mtu hutajwa kuwa maskini iwapo anapata Dola 700 pekee kwa mwaka.
Alisema kuwa lengo la mradi huo ni kusaidia zaidi ya asilimia 30 ya watu wanaoshi mashambani Kusini mwa Jangwa la Sahara ili wapate huduma ya kufuga kuku wa hali ya juu mbao watachanjwa. Alisema hatua hiyo itaongeza watu wanaofuga kuku kwa asilimia tano.
Ananukuliwa akisema kuwa kuku huongezeka maradufu na kwa hivyo hakuna uekezaji ulio na mapato mazuri kwa asilimia ya juu kuliko ufugaji kuku.
Alisema hayo alipokuwa akianzisha mradi huo jijini New York. Anashirikiana na shirika na kutoa misaada kwa maskini la Heifer International.
Watu milioni 800 huishi katika hali ya umaskini hohehahe, kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa.

Aliyewaua watu Florida alikiri kuunga IS mkono


Aliyewaua watu Florida alikiri kuunga IS mkono


Image copyrightREUTERS
Image captionOmar Mateen

Shirika la ujasusi la Marekani- FBI, limesema mtu aliyewaua watu 50 kwa kuwafyatulia risasi katika klabu moja ya wapenzi ya jinsia moja huko Florida, alikiri kuunga mkono kundi la kigaidi la IS, lakini hawakumuona kama mtu hatari.
Mateen, anasemekana kupigia simu mamlaka ya kitaifa ya maswala ya dharura muda mfupi kabla ya kuanza kuwapiga watu risasi huku akisema kuwa anaunga mkono kundi la IS.
FBI wameongeza kusema kuwa wamekuwa wakimfanyia uchunguzi mtu huyo tangu 2013 baada ya kutoa matamshi ya chuki akiwa kazini.

Image copyrightEPA
Image captionEneo la mkasa

Wakati alipotoa matamshi hayo ya chuki, alikuwa na uhusiano na mhanga mmoja aliyejilipua nchini Syria.
Mateen aliendelea kufanya kazi kama mlinzi wa usalama huku akinunua silaha kisheria.
Babake Mateen amesema anaamini kitendo alichokifanya mwanawe kilitokana na msukumo wa hisia zake dhidi ya wanaondeleza mapenzi ya jinsia moja na wala si kwa sababu za kidini.

Magufuli awaapisha Nchemba na Tizeba


Magufuli awaapisha Nchemba na Tizeba
Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewaapisha mawaziri wapya wa mambo ya ndani na yule wa kilimo siku mbili tu baada ya kutangaza mabadiliko madogo katika baraza lake la mawaziri.
 

Jumamosi iliyopita rais Magufuli alitangaza uteuzi wa mbunge wa Buchosha Dkt. Charles John Tizeba kuwa waziri wa kilimo, mifugo na uvuvi.
Kufuatia uteuzi huo, aliyekuwa Waziri wa Kilimo, bwana Mwigulu Lameck Nchemba aliteuliwa kuwa Waziri wa mambo ya ndani ya nchi.
Image captionRais Magufuli ampongeza waziri Nchemba kwa wadhifa wake mpya
Bwana Nchemba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani bw Charles Muhangwa Kitwanga ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.
Mawaziri hao walikula kiapo cha uaminifu kwa rais na jamhuri ya tanzania saa tatu asubuhi katika ikulu ya rais jijini Dar es salaam.

Harmonize Ft Diamond Platnumz Kwangwaru