Vurugu zimetokea katika mji wa Hong kong,kitongoji cha Mong
kok wakati polisi wakifanya operesheni katika maduka yanayouza vyakula haramu.
Fujo hizo zilianza wakati wataalamu wa usafi na chakula
walipojaribu kuondoa vibanda ambavyo vilikuwa barabarani, wafanyabiashara wenye
hasira kali walianza kurushia mawe polisi na kuwasha moto barabarani ili
kupinga kitendo hicho.
Hong kong ambayo bado inasheherekea sherehe za mwaka mpya
zilizoanza jana na kuchukua siku tatu za mapumziko. Maduka ya mitaani yanayouza
vyakula na vinyaji ni kawaida kwa wao kuuza bidhaa bila kuwa na vibali halali.
No comments:
Post a Comment