Watu walioshuhudia tukio hilo wanasema mwanamume huyo
alikuwa amepoteza $300 akicheza kamari.
Alijaribu kumsihi msimamizi wa kasino hiyo aruhusiwe kuweka
rehani simu yake lakini akakatazwa kwa msingi kuwa haikuwa imefikisha thamani
ya kuwekwa rehani, walioshuhudia wanasema.
Ni hapo ambapo anadaiwa kumdunga kisu msimamizi huyo wa
kasino mtaa wa Eastleigh.
Mlinzi wa msimamizi huyo alipomkabili, naye pia akamdunga
kisu na kumuua.
Baadaye alizidiwa nguvu na umati na kuuawa.
Polisi wamesema mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 28
anatoka eneo la Rombo, mkoa wa Kilimanjaro, Tanzania.
Alikuwa akifanya kazi kama fundi wa viatu kabla ya kuanza
biashara ya uchukuzi wa kutumia pikipiki, maarufu kama bodaboda nchini Kenya.
Kabla ya kisa hicho, waliokuwa wakifanya kazi naye wanasema
alikuwa ameuza pikipiki hiyo.
No comments:
Post a Comment