June 10, 2016

NAMNA YA KUPATA MTAJI WA KUANZISHA BIASHARA YAKO

                                        
NAMNA YA KUPATA MTAJI WA KUANZISHA BIASHARA YAKO
 
Watu wengi hasa vijana wanatamani wangeweza kujiajiri wenyewe wakiwa bishara zao binafsi. Hata hivyo sio wote wanaofanikiwa katika hilo kutokana na changamoto mbali mbali wanazokutana nazo. Mojawapo ya changamoto hizo ni namna ya kupata mtaji wa kuweza kuanzisha shughuli unayohitaji kuifanya. Kwenye makala hii tutaangalia namna ya kupta mtaji wa kuanzisha bishara yako kirahisi.
Kwanza kabisa kabla hujaanza kutafuta mtaji wa biashara yako kuna maswali ya msingi unayotakiwa kuyajibu kama:
1.             Ninahitaji nini ili BIASHARA YANGU IANZE?
2.             Nina rasilimali gani zitakazo wezesha biashara yangu ianze kama fedha, ofisi au vifaa vya kufanyia kazi?
3.             Naweza kupata wapi vifaa vya kufanyia kazi kwa gharama nafuu au bila gharama?
4.             Ninahitaji shilingi ngapi ili biashara yangu ianze?
5.             Nitapata wapi fedha za ziada ili kuanzisha biashara yangu?
Baada ya kujibu maswali yaliyopo hapo juu sasa tuangalie njia zitakazo kuwezesha wewe kupata mtaji wa kuaznisha biashara yako.
Akiba yako binafsi.
Hii ndio njia ya kwanza kabisa ya kupata mtaji wa kuanzisha biashara yako binafsi. Hata unapokwenda kukopa au kumshirikisha mtu biashara yako ni wazi kabisa atahitaji kujua jinsi ulivyojipanga hivi ndivyo hata mshirika ya kifenda yanavyofanya. Unapotumia fedha yako inakuongezea nidhamu kwenye biashara yako. Unaweza kuweka akiba kutokana na mshahara, fedha za matumizi kwa wanafunzi au fedha kutoka kwenye kazi fulani uliyoifanya. Unaweza kihifadhi fedha zako kwenye akaunti ya benki au kibubu. Zipo akaunti nzuri ya benki zisizo na makato ya mwezi na hutoa riba kuanzia kiasi Fulani cha kiba ili kusaidia kukuza mtaji wako. Ni vizuri ukiweza kuwekeza angalau asilimia 30-50 au zaiidi kwenye biashara yako. Hii pia inathibitisha nia yako ya kufanya biashara.
Ndugu jamaa na marafiki.
Baada yaw ewe mwenyewe kinachofuata sasa ni kuwasirikisha ndugu, jamaa au marafaiki wanaoweza kukusaidia kuanzisha biashara yako. Wanaweza kukuazima kiasi cha fedha, vifaa au mahali pa kufanyia biashara yako. Hakikisha umepiga mahesabu muhimu kabla ya kuazima na kuahidi muda wa kurudisha fedha au vifaa ulivyoazima, hii itakusaidia kutotofautiana na watu wanaokuazima fedha za kuendesha biashara yako amabao unawez kuwahitaii tena siku za usoni unapohitaji kukuza biashara yako. Hata hivyo inapotokea kuwa unashidwa kuwasilisha fedha kwa wakati ni vizuri kuwaataarifu mapema kwa kuwapigia simu au ukiweza kwenda kuwaona mwenyewe ni vizuri zaidi, sio ujumbe wa simu ili uweze kujenga imani kwao na kuonesha kuwa unajali mchango wao kwako.

Badilisha mali zako usizozitumia au au zisizo za muhimu kuwa fedha.
Inawezekana unamiliki simu ya gharama kubwa wakati mwingine zaidi ya simu moja, ipad, ipod na vifaa vingine vinavyofanana na hivyo. Unaweza kuviuza hivyo kwa mtu anayehitaji ili upata mtaji wa kuanzisha bbiashara yako.  Ni rahisi kwa vifaa kama hivi kushikilia fedha ya kuanzisha biashara yako, ukizingatia kuwa wakati mwingine vinakuwa na kazi moja,  kwa mfano unaweza kusikiliza muziki kwa kutumia simu na kuuza ipod yako.
Tumia sehemu ya mkopo wa chuo kikuu.
Wapo watu wengi sana wanaonufaika na mikopo ya elimu ya juu kwa ajili ya kugharamia masomo yao. Fedha hizi zimewawezesha vijana wengi kujiairi na wengine hata kujenga nyumba za kuanzia maisha au kununua viwanja na mashamba kutokana na kuwekeza sehemu ya fedha hizo. Wapo watu wengi pia wanaolalamika kutoteosheka na fedha hizo wanazopewa hata hivyo ukiangalia kwa makini utagundua kuwa tatizo ni vipaumbele walivyojiwekea.
Jiunge na mfuko wa kukuza fedha wa UTT.
Mfuko huu wa kukuza fedha ni njia nzuri ya kukuza fedha kwa ajili ya kupata fedha za kuanzisha biashara yako. Hata ni wa muda mrefu kidogo hivyo unatakiwa uutumie kwa malengo ya muda mrefu kama mwaka au zaidi. Unapoweka fedha kwenye mfuko huu wa hisa za pamoja unapata riba ya kila mwezi uanpo weka fedha. Pia hakuna gharama za kila mwezi wala makato yoyote.

No comments:

Post a Comment

Harmonize Ft Diamond Platnumz Kwangwaru