Magufuli
awaapisha Nchemba na Tizeba
Rais
wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewaapisha mawaziri wapya wa mambo ya
ndani na yule wa kilimo siku mbili tu baada ya kutangaza mabadiliko madogo
katika baraza lake la mawaziri.
Jumamosi
iliyopita rais Magufuli alitangaza uteuzi wa mbunge wa Buchosha Dkt. Charles
John Tizeba kuwa waziri wa kilimo, mifugo na uvuvi.
Kufuatia
uteuzi huo, aliyekuwa Waziri wa Kilimo, bwana Mwigulu Lameck Nchemba aliteuliwa
kuwa Waziri wa mambo ya ndani ya nchi.
Image captionRais
Magufuli ampongeza waziri Nchemba kwa wadhifa wake mpya
Bwana
Nchemba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani
bw Charles Muhangwa Kitwanga ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.
Mawaziri
hao walikula kiapo cha uaminifu kwa rais na jamhuri ya tanzania saa tatu
asubuhi katika ikulu ya rais jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment