MAMBO SITA YA KUZINGATIA WAKATI WA UCHAGUZI ENEO LA BUSTANI
Kwa
mafanikio ya kilimo cha bustani ni muhimu sana kuzingatia uchaguzi wa
eneo, hii itapelekea zao Fulani kutoa mazao mazuri kutokana na uchaguzi
mzuri wa eneo, kwa kuzingatia sifa zifuatazo za eneo hilo.
Chagua eneo lenye sifa zifuatazo.
1.HALI YA HEWA.
Hali
ya hewa hapa vipengele vifuatavyo vinahusishwa joto (Temperature), mvua
(rainfall) kiasi cha unyevu katika anga (humidity), kasi ya upepo
(wind), zote hizi ni vitu vya kuzingatia sana katika uchaguzi wa eneo,
mazao mengi yana mahitaji tofauti ya hali ya hewa hivyo kukufanya ewe
mkulima kuwa mwangalifu katika hill.
2.AINA YA ZAO
Aina ya zao
pia ni kitu kingine cha muhimu sana, mazao na eneo hupelekea mafaniio ya
kilimo sio mazao yote yanaleta fauda kubwa hivyo chagua zao ambalo
litaendana na faida kwa kushirikisha na uchaguzi wa eneo pamoja na soko
lako.
3.CHANZO CHA MAJI.
Maji ni uhai wa bustani na maji hayo
yawe na sifa zifuatazo yawe yanapatikana kwa kipindi chote cha msimu wa
uzalishaji, maji yawe yenye ubora na sio yaliyo changanyika na kemikali,
ambazo huenda yakaleta madhara kwa matumizi ya binadamu.
4.UPATIKANAJI WA VIBARUA.
Wafanyakazi kwaajili ya kufanya shughuli mbalimbali za shamba ikiwemo palizi, upuliziaji wa dawa shamba na hata uvunaji.
5.URAHISI KUFIKA SOKONI.
Ufikaji wa mazao sokoni ni jambo pia la kuzingatia, kuanzia usafirishaji.
6.AINA YA UDONGO.
Kila
zao lina aina yake ya udongo kwaajili uzalishaji utakaoleta mazao
mazuri, hivyo zingatia sana aina ya udongo, kuna aina kuu tatu za udongo
mfinyanzi, kichanga, na tifutifu,
Udongo wa mfinyanzi hufaa sana
mazao kama kitunguu, mpunga kwani udongo huu hutuamisha sana maji,
udongo wa kichanga hufaa kwa mazao kama karroti, udongo wa tifutifu huu
ni udongo ambao mazao mengi hustawi sana kwani ndio udongo unaoshauriwa
sana kitaalamu kwa mavuno bora.
No comments:
Post a Comment