June 13, 2016

'Waislamu hawafai kuingia Marekani' -Trump


'Waislamu hawafai kuingia Marekani' -Trump

Image copyrightAP
Image caption'Waislamu hawafai kuingia Marekani' -Trump
Mgombea wa kiti cha urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump, amesema mauaji ya watu 50 katika baa moja ya wapenzi wa jinsia moja huko Orlando inathibitisha msimamo wake kwamba waislamu wapigwe marufuku kukanyaga ardhi ya Marekani.
Trump amemkashifu mpinzani wake wa chama cha republican Bi Hillary Clinton, kwa kutodadisi sababu za mtu huyo kutenda mauaji hayo.
Image copyrightTWITTER
Image captionTrump amesema hatua kali zinapaswa kuchukuliwa dhidi ya waislamu
Upande wa Bi Clinton wakitoa risala za pole kwa waathiriwa wa mkasa huo papo hapo wamemtaja Trump kama mtoto anaejitweza ovyo kwa jinsi anavyougeuza mkasa huo wa kitaifa kujipongeza binafsi.
Image copyrightGETTY
Image captionWakati huo huo Shirika la kijasusi la FBI limesema mtu aliyewaua watu 50 kwa kuwafyatulia risasi katika klabu moja ya wapenzi ya jinsia alikiri kuunga mkono kundi la kigaidi la IS.
Wakati huo huo Shirika la kijasusi la FBI limesema mtu aliyewaua watu 50 kwa kuwafyatulia risasi katika klabu moja ya wapenzi ya jinsia alikiri kuunga mkono kundi la kigaidi la IS.
Image copyrightEPA
Image captionWatu 50 waliuawa katika shambulizi la risasi
Fbi wameongeza kusema kuwa wamekuwa wakimfanyia uchunguzi mtu huyo Omar Mateen tangu 2013 baada ya kutoa matamshi ya chuki akiwa kazini .
Image copyrightAFP
Image captionTrump amemkashifu mpinzani wake Hillary Clinton kwa utepetevu
Babake Mateen amesema anaamini kitendo alichokifanya wanawe kilitokana na msukumo wa hisia zake dhidi ya wanaondeleza mapenzi ya jinsia moja na wala si kwa sababu za kidini.
Naye mkewe wa zamani Sitora Yusufiy, amemwelezea Mateen kama mtu wa aliyekuwa tabia za kigomvi na kutaka kupiga watu lakini hakuwa na itikadi kali za kidini.

Bill Gates kusaidia watu kufuga kuku Afrika


Bill Gates kusaidia watu kufuga kuku Afrika

Mwanzilishi wa kampuni ya Microsoft Bill Gates, amezindua kampeni ya kusaidia watu maskini zaidi barani Afrika, kusini mwa jangwa la sahara, kwa kufuga kuku
Bilionea huyo Bill Gates anasema kuwa kufuga kuku kunaweza kuwa kifaa muhimu katika kukabiliana na ufukara hohe hahe.
Ameahidi kutoa kuku 100,000, na ukurasa katika mtandao wa mradi huo tayari umewavutia na kusambazwa kwa maelfu ya watu.
Umoja wa Mataifa unakisia kuwa asilimia 41 ya watu katika Bara la Afrika, Kusini mwa jangwa la Sahara wanaishi katika ufukara mkubwa.
Image captionBwana Gates alisema kuwa mkulima anayefuga kuku watano anaweza kupata zaidi ya Dola 1,000 kwa mwaka.
Bwana Gates alisema kuwa mkulima anayefuga kuku watano anaweza kupata zaidi ya Dola 1,000 kwa mwaka. Mtu hutajwa kuwa maskini iwapo anapata Dola 700 pekee kwa mwaka.
Alisema kuwa lengo la mradi huo ni kusaidia zaidi ya asilimia 30 ya watu wanaoshi mashambani Kusini mwa Jangwa la Sahara ili wapate huduma ya kufuga kuku wa hali ya juu mbao watachanjwa. Alisema hatua hiyo itaongeza watu wanaofuga kuku kwa asilimia tano.
Ananukuliwa akisema kuwa kuku huongezeka maradufu na kwa hivyo hakuna uekezaji ulio na mapato mazuri kwa asilimia ya juu kuliko ufugaji kuku.
Alisema hayo alipokuwa akianzisha mradi huo jijini New York. Anashirikiana na shirika na kutoa misaada kwa maskini la Heifer International.
Watu milioni 800 huishi katika hali ya umaskini hohehahe, kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa.

Aliyewaua watu Florida alikiri kuunga IS mkono


Aliyewaua watu Florida alikiri kuunga IS mkono


Image copyrightREUTERS
Image captionOmar Mateen

Shirika la ujasusi la Marekani- FBI, limesema mtu aliyewaua watu 50 kwa kuwafyatulia risasi katika klabu moja ya wapenzi ya jinsia moja huko Florida, alikiri kuunga mkono kundi la kigaidi la IS, lakini hawakumuona kama mtu hatari.
Mateen, anasemekana kupigia simu mamlaka ya kitaifa ya maswala ya dharura muda mfupi kabla ya kuanza kuwapiga watu risasi huku akisema kuwa anaunga mkono kundi la IS.
FBI wameongeza kusema kuwa wamekuwa wakimfanyia uchunguzi mtu huyo tangu 2013 baada ya kutoa matamshi ya chuki akiwa kazini.

Image copyrightEPA
Image captionEneo la mkasa

Wakati alipotoa matamshi hayo ya chuki, alikuwa na uhusiano na mhanga mmoja aliyejilipua nchini Syria.
Mateen aliendelea kufanya kazi kama mlinzi wa usalama huku akinunua silaha kisheria.
Babake Mateen amesema anaamini kitendo alichokifanya mwanawe kilitokana na msukumo wa hisia zake dhidi ya wanaondeleza mapenzi ya jinsia moja na wala si kwa sababu za kidini.

Magufuli awaapisha Nchemba na Tizeba


Magufuli awaapisha Nchemba na Tizeba
Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewaapisha mawaziri wapya wa mambo ya ndani na yule wa kilimo siku mbili tu baada ya kutangaza mabadiliko madogo katika baraza lake la mawaziri.
 

Jumamosi iliyopita rais Magufuli alitangaza uteuzi wa mbunge wa Buchosha Dkt. Charles John Tizeba kuwa waziri wa kilimo, mifugo na uvuvi.
Kufuatia uteuzi huo, aliyekuwa Waziri wa Kilimo, bwana Mwigulu Lameck Nchemba aliteuliwa kuwa Waziri wa mambo ya ndani ya nchi.
Image captionRais Magufuli ampongeza waziri Nchemba kwa wadhifa wake mpya
Bwana Nchemba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani bw Charles Muhangwa Kitwanga ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.
Mawaziri hao walikula kiapo cha uaminifu kwa rais na jamhuri ya tanzania saa tatu asubuhi katika ikulu ya rais jijini Dar es salaam.

June 11, 2016

MAMBO YANAYOWAKWAMISHA WAJASIRIAMALI


MAMBO  YANAYOWAKWAMISHA WAJASIRIAMALI

  Tunaishi kwenye zama ambazo ni muhimu sana kwa mtu kuwa mjasiriamali. Hii ni kwa sababu kumekuwa na mabadiliko makubwa sana kiuchumi ambayo yametoa nafasi kwa watu kuweza kuingia kwenye ujasiriamali na kufanikiwa. Ukosefu wa ajira na pia changamoto wanazopata watu kwenye ajira zinawasukuma watu kuingia kwenye ujasiriamali. Pia maendeleo ya kiteknolojia yamerahisisha sana ujasiriamali. Kukua kwa mtandao wa intaneti na uwepo wa mitandao ya kijamii umefanya mtu kuweza kuuza bidhaa au huduma zake katika mataifa ya mbali bila ya yeye kusafiri au kutumia gharama kubwa. 
Pamoja na mazingira haya mazuri yanayowavutia watu kuingia kwenye ujasiriamali bado sio wote wanaoingia kwenye ujasiriamali wanapata mafanikio makubwa na hata kukua. Ukweli ni kwamba watu wengi wanaoingia kwenye ujasiriamali au wanaoanza biashara, biahsara zao zinaishia kufa ndani ya muda mfupi. Hata wale ambao biashara zao hazifi, zinaishia kudumaa na kushindwa kukua zaidi. Kuna watu wengi ambao wamekuwa wanafanya biashara ya aina moja miaka mingi bila ya kuona mabadiliko makubwa kwao na kwa biashara wanayofanya. 
Leo, hapa
  tutajadili vikwazo mbalimbali vilivyopo kwenye safari ya ujasiriamali na jinsi ambavyo unaweza kuvivuka ili uweze kufikia mafanikio makubwa kupitia ujasiriamali wako. 
Vifuatavyo ni vikwazo vilivyopo kwenye safari ya ujasiriamali vinavyowazuia wajasiriamali wengi kushindwa kufikia mafanikio makubwa.
 
i) Mtazamo wa mjasiriamali mwenyewe 
Watu wengi wanapofikiria kuingia kwenye biashara au ujasiriamali huamini kwamba wanakuwa mabosi wao wenyewe na hivyo hakuna wa kuwapelekesha. Hakuna mtu anayeweza kuwafanya waamke asubuhi na mapema kutekeleza majukumu yao, wafanye kazi muda wa ziada au hata kufanya vitu wasivyopenda kufanya. Kwa mtazamo huu mjasiriamali anayeanza anakuwa anafanya mambo kwa muda anaojisikia mwenyewe na hivyo kushindwa kuwa na uzalishaji mkubwa. Unapoingia kwenye ujasiriamali, hasa wakati wa mwanzoni unahitaji kufanya kazi zaidi hata ya mtu ambaye ameajiriwa. Mtu aliyeajiriwa anafanya kazi masaa nane mpaka kumi kwa siku na siku tano kwa wiki. Mjasiriamali anaweza kujikuta anafanya kazi masaa zaidi ya kumi na mbili kwa siku na wakati mwingine siku saba kwa wiki. Kufikiri kwamba kuwa kwenye ujasiriamali au biashara ni kufanya kile unachojisikia kufanya kwa wakati unaomamua mwenyewe ni kikwazo kikubwa cha watu wengi kufanikiwa kwenye ujasiriamali.
 


ii) Ushindani mkali 
Changamoto nyingine wanayoipata wajasiriamali ni ushindani mkali ambao wanakutana nao wanapoingia kwenye biashara. Mara nyingi watu wanapoingia kwenye biashara kwa mara ya kwanza huangalia ni biashara gani inalipa na wao kujiingiza kwenye biashara kama hiyo. Unapokuwa nje na kabla ya kuingiakwenye biashara unaweza kuona inalipa vizuri sana. Unaweza kuweka mipango mikubwa na mizuri sana na kuona ukiingia ni jinsi gani unaweza kupata faida kubwa. Ila unapoingia kwenye biashara husika ndipo unapokutana na ukweli ambao hukuweza kuuona mwanzoni wakati unapanga. Unapoingia kwenye biashara unaona jinsi ambavyo ushindani ni mkubwa na wale ambao wamekutangulia wanakuwa na uwezo mkubwa wa kuhimili ushindani huo kuliko wewe unayeanza. Hii imekuwa ikiwafanya wengi wanaoingia kwenye biashara kushindwa na hatimaye kluacha kabisa biashara hiyo.
 
iii) Mtazamo wa wanaokuzunguka 
Kuwa mjasiriamali au mfanyabiashara kwenye mazingira ya nchi masikini kama Tanzania, kila mtu anaangalia jinsi ya kukurudisha nyuma. Hii ni kwa sababu kila mtu anapenda kupata zaidi kwa gharama kidogo. Hivyo unaweza kuanza biashara kwa kushirikiana na mtu au watu wengine na wao wakataka kufaidi kuliko unavyofaidi wewe. Unaweza kuajiri wa fanyakazi na wao wakawa ndio watu wa kwanza kukuibia. Na hata ndugu zako wa karibu wanapoona unafanya biashara wanaweza kuamini kwamba wewe unapata faida kubwa na hivyo kutegemea wewe uwasaidie. Mambo haya ni changamoto kubwa sana hasa mwanzoni mwa biashara ambapo unahitaji kukua zaidi ya kuondoa fedha kwenye biashara.
 
iv) Kufanya vitu kwa mazoea na kutokupenda kujifunza 
Ujasiriamali unahitaji kujifunza kila siku na kuwa mbunifu kila mara. Watu wengi hawapendi kusumbua vichwa vyao kufikiri zaidi. Wanapenda kufanya kile ambacho wamezoea kufanya, wanapenda kufanya walichofanya jana. Hii inawafanya kuingia kwenye changamoto kubwa sana ya kushindwa kubadilika kadiri mazingira yanavyobadilika. Kwa kushindwa kubadilika wanazidi kubaki nyuma na kujiweka katika nafasi ya kuweza kushindwa pale unapotokea ushindani.
 
Kujifunza kila siku ni hitaji muhimu sana ili kuweza kufanikiwa kwenye biashara na ujasiriamali. Dunia ya sasa mambo yanabadilika kwa kasi kubwa sana. Kuna taarifa muhimu sana unazotakiwa kuzipata kuhusiana na biashara unayofanya na hata biashara kwa ujumla. Utazipata taarifa hizi kama unapenda kujifunza na hata kusoma mambo yanayoendana na biashara.
 

v) Matatizo ya kifedha 
Fedha ndio damu ya biashara yoyote ile, kama ilivyo damu kwenye mwili wa binadamu. Mzunguko mzuri wa fedha kwenye biashara ndio utaifanya biashara iwe hai na iendelee kukua. Matatizo yoyote kwenye mzunguko wa fedha yanaweza kupelekea kufa kwa biashara kama ambavyo mtu atakufa kama akipatwa na matatizo makubwa kwenye mfumo wake wa damu.
 
Wafanyabiashara wengi wamekuwa wanashindwa kutofautisha matumizi yao binafsi na matumizi ya biashara zao. Hivyo wamekuwa wakitumia fedha inayotoka kwenye biashara moja kwa moja na hivyo kutumia kile wanachozalisha. Hii inawafanya kushindwa kujua kama wanatengeneza faida au wanapata hasara na mwishowe wanashindwa kujua kama wanakua, wamedumaa au wanarudi nyuma.
 
Changamoto hizi zimekuwa kikwazo kikubwa kwenye maendeleo ya ujasiriamali na biashara. Na kama tulivyoona kwenye changamoto hizo, nyingi zinaweza kuzuilika au kuondolewa kabisa na mfanyabiashara akaweza kuona faida kutokana na biashara anayofanya.
 
Msomaji wa
 ngu, yafuatayo ni baadhi ya mambo ambayo mfanyabiashara anaweza kufanya ili kuepuka changamoto zinazoweza kumwondoa kwenye biashara. 
1. Jua kwamba biashara au ujasiriamali ndio kazi yako na inakuhitaji sana ili kukua 
Kama upo kwenye ujasiriamali au unapanga kuingia kwenye ujasiriamali ni muhimu kujua kabisa ya kwamba safari hii ya ujasiriamali sio rahisi. Ni safari ambayo inahitaji wewe kujitoa, uwe tayari kufanya kazi kwa muda mrefu zaidi ya watu walioajiriwa na uwe tayari kufanya kazi nyingi zaidi ya mtu aliye kwenye ajira. Unapoanzisha biashara yakounaweza kuvaa kofia nyingi sana kwa wakati mmoja, unaweza kuwa wewe ndio mmiliki wa biashara, wewe ndio afisa masoko, wewe ndio mhasibu, wewe ndio mtafiti na wewe ndio afisa mauzo. Ni lazima uyajue maeneo yote muhimu ya biashara yako ili kujua ni wapi panahitaji nguvu zaidi ili uweze kukua zaidi. Ni lazima uweze kujidukuma kufanya kazi hata pale ambapo hujisikii kufanya hivyo. Na jambo muhimu sana kwenye safari ya ujasiriamali ni kwamba unahitaji kuweza kujiongoza mwenyewe. Usiwe ni mtu ambaye unasubiri kupangiwa nini cha kufanya au kusukumwa ndio uweze kutekeleza majukumu yako.
 
2. Kuwa mbunifu na jitofautishe na wengine 
Unaweza kuingia kwenye biashara kwa kuangalia ni biashara gani inayotoka kwa maeneo unayotaka kufanyia biashara ila usitegemee biashara yako kukua kwa kufanya kile ambacho kila mtu anafanya. Unahitaji kuwa na ubunifu mkubwa na kuweza kujitofautisha na wafanyabiashara wengine wanaofanya biashara kama unayofanya wewe. Fikiria jinsi ambavyo unaweza kufanya biashara yako tofauti na ukawavutia wateja wengi zaidi. Angalia ni vitu gani ambavyo ni muhimu kwa ukuaji wa biashara hiyo na ambavyo wafanya biashara wengine hawavifanyi kisha vifanye. Hii itakufanya wewe kuwa wa pekee na hivyo kuondoka kwenye ushindani ambao utakuumiza kichwa. Katika kila biashara kuna jambo linaloweza kuboreshwa zaidi na kuifanya biashara kukua zaidi.
 
3. Shirikiana na watu ambao unaweza kuwaamini na wanapenda kufanya biashara unayofanya 
Kama unahitaji kushirikiana na mtu ili kuanzisha biashara hakikisha unashirikiana na mtu ambaye unamjua vizuri na unaweza kumuamini. Mtu huyo awe na rekodi nzuri ya kufanya mambo kwa uaminifu ili muweze kuaminiana kwenye biashara. Na pale unapoajiri ajiri watu wenye uwezo, waaminifu na ambao wanapenda kufanya biashara hiyo ambayo unawaajiri. Kuajiri mtu ambaye anataka tu kupata mshahara atakuwa mzigo kwako hasa kwenye kipindi ambapo biashara inakuwa ngumu.
 
4. Kuwa na usimamizi mzuri wa fedha kwenye biashara yako 
Cha kwanza kabisa kwenye usimamizi wa fedha za biashara yako, itofautishe biashara yako na wewe binafsi. Matumizi ya biashara yafanye tofauti kabisa na matumizi yako binafsi. Jua mauzo ya biashara yako na faida unayoipata baada ya kuondoa matumizi yote ya biashara. Pia matumizi yako yaweke kwenye biashara kama mshahara ambao unajilipa. Hii itakufanya uweze kuona kama biashara yako inakua au inadidimia.
 
5. Kuwa mvumilivu 
Hakuna kitu chochote unachoweza kufanikiwa kwenye maisha kama hutakuwa na uvumilivu. Utakutana na vikwazo vingi sana kwenye safari yako ya biashara. Kuna wakati ambapo utaona unashindwa kabisa ila unapokata tama ndio unakubali kujiondoa kwenye njia ya mafanikio. Kuwa mvumilivu na jifunze kupitia changamoto unazopata, kama kuna kitu umekosea na kikakugharimu jifunze kupitia kitu hiko na usikirudie tena. Jinsi unavyokutana na changamoto nyingi ndio unazidi kujifunza na kukomaa.
 

Mafanikio kwenye ujasiriamali na biashara sio kitu ambacho kinatokea mara moja na kwa haraka. Ni kitu ambacho kinahitaji muda, kufanya kazi kwa bidii na maarifa na kuwa mvumilivu. Wafanyabiashara wakubwa tunaowaona leo hawakuanzia walipo sasa, walianzia chini kabisa na juhudi na uvumilivu ndio vimewafikisha

June 10, 2016

NAMNA YA KUPATA MTAJI WA KUANZISHA BIASHARA YAKO

                                        
NAMNA YA KUPATA MTAJI WA KUANZISHA BIASHARA YAKO
 
Watu wengi hasa vijana wanatamani wangeweza kujiajiri wenyewe wakiwa bishara zao binafsi. Hata hivyo sio wote wanaofanikiwa katika hilo kutokana na changamoto mbali mbali wanazokutana nazo. Mojawapo ya changamoto hizo ni namna ya kupata mtaji wa kuweza kuanzisha shughuli unayohitaji kuifanya. Kwenye makala hii tutaangalia namna ya kupta mtaji wa kuanzisha bishara yako kirahisi.
Kwanza kabisa kabla hujaanza kutafuta mtaji wa biashara yako kuna maswali ya msingi unayotakiwa kuyajibu kama:
1.             Ninahitaji nini ili BIASHARA YANGU IANZE?
2.             Nina rasilimali gani zitakazo wezesha biashara yangu ianze kama fedha, ofisi au vifaa vya kufanyia kazi?
3.             Naweza kupata wapi vifaa vya kufanyia kazi kwa gharama nafuu au bila gharama?
4.             Ninahitaji shilingi ngapi ili biashara yangu ianze?
5.             Nitapata wapi fedha za ziada ili kuanzisha biashara yangu?
Baada ya kujibu maswali yaliyopo hapo juu sasa tuangalie njia zitakazo kuwezesha wewe kupata mtaji wa kuaznisha biashara yako.
Akiba yako binafsi.
Hii ndio njia ya kwanza kabisa ya kupata mtaji wa kuanzisha biashara yako binafsi. Hata unapokwenda kukopa au kumshirikisha mtu biashara yako ni wazi kabisa atahitaji kujua jinsi ulivyojipanga hivi ndivyo hata mshirika ya kifenda yanavyofanya. Unapotumia fedha yako inakuongezea nidhamu kwenye biashara yako. Unaweza kuweka akiba kutokana na mshahara, fedha za matumizi kwa wanafunzi au fedha kutoka kwenye kazi fulani uliyoifanya. Unaweza kihifadhi fedha zako kwenye akaunti ya benki au kibubu. Zipo akaunti nzuri ya benki zisizo na makato ya mwezi na hutoa riba kuanzia kiasi Fulani cha kiba ili kusaidia kukuza mtaji wako. Ni vizuri ukiweza kuwekeza angalau asilimia 30-50 au zaiidi kwenye biashara yako. Hii pia inathibitisha nia yako ya kufanya biashara.
Ndugu jamaa na marafiki.
Baada yaw ewe mwenyewe kinachofuata sasa ni kuwasirikisha ndugu, jamaa au marafaiki wanaoweza kukusaidia kuanzisha biashara yako. Wanaweza kukuazima kiasi cha fedha, vifaa au mahali pa kufanyia biashara yako. Hakikisha umepiga mahesabu muhimu kabla ya kuazima na kuahidi muda wa kurudisha fedha au vifaa ulivyoazima, hii itakusaidia kutotofautiana na watu wanaokuazima fedha za kuendesha biashara yako amabao unawez kuwahitaii tena siku za usoni unapohitaji kukuza biashara yako. Hata hivyo inapotokea kuwa unashidwa kuwasilisha fedha kwa wakati ni vizuri kuwaataarifu mapema kwa kuwapigia simu au ukiweza kwenda kuwaona mwenyewe ni vizuri zaidi, sio ujumbe wa simu ili uweze kujenga imani kwao na kuonesha kuwa unajali mchango wao kwako.

Badilisha mali zako usizozitumia au au zisizo za muhimu kuwa fedha.
Inawezekana unamiliki simu ya gharama kubwa wakati mwingine zaidi ya simu moja, ipad, ipod na vifaa vingine vinavyofanana na hivyo. Unaweza kuviuza hivyo kwa mtu anayehitaji ili upata mtaji wa kuanzisha bbiashara yako.  Ni rahisi kwa vifaa kama hivi kushikilia fedha ya kuanzisha biashara yako, ukizingatia kuwa wakati mwingine vinakuwa na kazi moja,  kwa mfano unaweza kusikiliza muziki kwa kutumia simu na kuuza ipod yako.
Tumia sehemu ya mkopo wa chuo kikuu.
Wapo watu wengi sana wanaonufaika na mikopo ya elimu ya juu kwa ajili ya kugharamia masomo yao. Fedha hizi zimewawezesha vijana wengi kujiairi na wengine hata kujenga nyumba za kuanzia maisha au kununua viwanja na mashamba kutokana na kuwekeza sehemu ya fedha hizo. Wapo watu wengi pia wanaolalamika kutoteosheka na fedha hizo wanazopewa hata hivyo ukiangalia kwa makini utagundua kuwa tatizo ni vipaumbele walivyojiwekea.
Jiunge na mfuko wa kukuza fedha wa UTT.
Mfuko huu wa kukuza fedha ni njia nzuri ya kukuza fedha kwa ajili ya kupata fedha za kuanzisha biashara yako. Hata ni wa muda mrefu kidogo hivyo unatakiwa uutumie kwa malengo ya muda mrefu kama mwaka au zaidi. Unapoweka fedha kwenye mfuko huu wa hisa za pamoja unapata riba ya kila mwezi uanpo weka fedha. Pia hakuna gharama za kila mwezi wala makato yoyote.

Harmonize Ft Diamond Platnumz Kwangwaru