Shinikizo lakumtaka Rais Jacob Zuma ajiuzulu lazidi kuongezeka
![]() |
| Cyril Ramaphosa & Jacob Zuma |
Shinikizo linaongezeka dhidi ya rais
Jacob Zuma Afrika kusini kujiuzulu, huku maafisa wakuu kutoka chama tawala ANC
wakitarajiwa kukutana naye Jumapili kujadili mustakabali wake.
Rais Zuma anakabiliwa na tuhuma za
rushwa na jitihada za wapinzani na baadhi ya wafuasi wa ANC wanaotaka kumtimua
madarakani.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi, maafisa
wa ngazi ya juu wa ANC wana 'jadiliana tu' na rais Zuma kuhusu "ugavi wa
uongozi" ndani ya chama.
Lakini nyuma ya kauli hiyo nyepesi -
vita vikali vya uongozi vinajitokeza katika nchi hiyo.
Rais Zuma bado yupo madarakani,
lakini tangu Desemba mwaka jana, yeye sio mkuu tena wa ANC.
Haki miliki ya picha AFP Image
caption Kiongozi mpya wa chama cha ANC - Ramaphosa, ameshutumu wazi rushwa
katika kiwango cha juu, ndani ya chama na pia serikali
Waendesha mashtaka wakakamavu sasa
wanaonekana kushika kasi katika uchunguzi dhidi ya tuhuma za rushwa
zinazomkabili bwana Zuma na baadhi ya marafaiki zake wa karibu.
Wengi ndani ya ANC wanamtaka rais
huyo ajiuzulu haraka iwezekanavyo, ili waweze kulenga kujenga upya sifa ya
chama hicho kufuatia kuwadia kwa uchaguzi mkuu nchini mwakani.
Lakini kuna taarifa kwamba Zuma
anajikita kisawasawa.
Anatarajiwa kulihotubia bunge wiki
ijayo, lakini wafuasi wa upinzani wanataka kumzuia pia, wakieleza kuwa
hastahili kusalia kama rais.
Kiongozi mpya wa ANC, Cyril
Ramaphosa, ameshutumu wazi rushwa katika kiwango cha juu ndani ya chama na
serikali, lakini anasisitiza kuwa rais Zuma hastahili kuazirishwa
